SEMINA YA LISHE BORA YAFANYIKA SHULENI HAPA IKIWA NA KAULI MBIU YA "WATOTO KWANZA, KWANZA WATOTO ,WAKUBWA BAADAE"

Kulia ni Daktari Nembris Andrea na Kushoto kwake ni Daktari Christina Urio kutoka Hospitali ya Sombetini, Ngusero Jijini Arusha, wakiendesha semina ya Lishe Bora na kuondoa UTAPIAMLO(MALNUTRITION) kwa watoto na watu wazima kwa ujumla. 
Semina hizi walifanya katika shule za serikali kabla ya kuja kwenye shule binafsi. Walifundisha jinsi ya kula , kutumia na kuandaa Vyakula mbali mbali kwa ufasaha ili kuondoa Utamiamlo na kujenga mwili kwa watu wote. 
Waliongeza kuwa Tanzania ni nchi ya Tatu (3) kwa UTAPIAMLO ,hivyo basi wanafunzi na waalimu wameaswa kupeleka elimu hiyo kwa wazazi wao na majirani ili kwa ujumla tuweze kutokomeza UTAPIAMLO Tanzania.
Pia walihimiza watu kula vyakula kama; Dagaa, ugali wa dona, mboga za majani(hasa Spinach) ,maziwa ,viazi na kutumia mafuta ya mimea. Pia walihimiza kupanda mboga mboga majumbani mwetu hata kwa wasio na sehemu za kupanda,walishauri wachukue mifuko ya simenti waweke udongo na wapande mboga hasa Spinach. Mwisho walikataza ulaji wa Chipsi na kunywa maji mara tu baada ya kula,walishauri angalao utumie maji au tunda saa moja kabla au baada ya kula na kuhakikisha chumvi tunayo tumia ina Madini Joto.
Mkuu wa shule Mr. Keya Wabuti aliesimama kulia akifurahia mafunzo ya Lishe Bora ....

Wanafunzi wakifuatilia kwa umakini semina ya Lishe Bora

Mwanafunzi akionyesha jinsi ya kuandaa mboga za majani kabla ya kupika...

Waalimu na wanafunzi wakifuatilia kwa ufasaha semina ya Lishe Bora...
Wanafunzi na waalimu wakifuatilia kwa ufasaha semina ya Lishe Bora...


Mwanafunzi wa darasa la Kwanza akionyesha jinsi ya kuandaa mboga za majani (hasa majani ya maboga) kabla ya kupika...


UTAPIAMLO ni Ukosefu wa Virutubishi mwilini.
HADY SCHOOLS

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post