Kaimu
Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dk. Adolf
Rutayuga, (Kulia) akisisitiza jambo wakati alipokuwa ikitangaza wa
kuzindua Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)) kwa
mafunzo yanayoratibiwa na Baraza kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Mfumu
huo, utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada
(Cheti), Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (“Bachelor Degree)
Katikati ni Mkurugenzi Udhibiti Ubora Rasmalimali watu , Edmund Kinwasi
na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ufuatiliaji Tathimini na Uthibiti wa
baraza hilo , Christina Kumwenda. Uzinduzi huo ulifanyika leo jijini Dar
es Salaam.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dk .Adolf
Rutayuga, akipofya kitufe cha komputa kuashiria Uzinduzi rasmi wa
Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)) kwa mafunzo
yanayoratibiwa na Baraza kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Mfumu huo,
utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada (Cheti),
Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (“Bachelor Degree)
wanaoshuhudia kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ufuatiliaji
,Tathimini na Uthibiti ,Christina Kumwenda, Mkurugenzi udhibiti ubora
rasmalimali watu Edmund Kinwas, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Vyuo
ushauri na Mipango Alfred Kilasi,Mkurugenzi Mafunzo na Upimaji Bakari
Issa (kushoto) na Afisa Mifumo ya Kompyuta wa baraza hilo , Daud
Mabena.Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt .Adolf
Rutayuga(Kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini
Dar es Salaam ( hawapo pichani) kuhusiana na Uzinduzi wa Mfumo wa
Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)) kwa mafunzo
yanayoratibiwa na Baraza kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Mfumu huo
utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada (Cheti),
Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (“Bachelor Degree) wapili
kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Udahili Seremani Majindo, Mkurugenzi wa
Mfumo na Upimaji,Bakari Issa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya vyuo na
ushauri na Mipango.Uzinduzi huo ulifanyika leo jijini Dar es Salaam
BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), limetangaza ufunguzi rasmi wa
Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)) kwa mafunzo
yanayoratibiwa na Baraza kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Mfumu huo, utatumika
kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada (Cheti), Stashahada
(Diploma) na Shahada ya kwanza (“Bachelor Degree”).
Akizungumza
na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Maelekezo na
Msaada kwa Taasisi wa NACTE, Dk. Adolf Rutayuga amesema kuwa, kwa mwaka wa masomo wa 2015/16, Baraza liliratibu udahili wa wanafunzi
katika vyuo mbali mbali kwa kozi za astashahada (Cheti) na stashahada (Diploma)
kwa mafunzo ya afya na ualimu yaliyoidhinishwa na Baraza. ameongeza kuwa,
Baraza pia lilishirikiana na Tume ya
Vyuo Vikuu Tanzania, kuratibu udahili wa wanafunzi katika vyuo mbali mbali kwa
kozi za shahada ya kwanza kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission
System (CAS)).
“Mifumo hii miwili ilifanyika kwa ufanisi mkubwa na uliwawezesha waombaji kudahiliwa. Mifumo hii ya udahili
imekuwa na mafanikio yafuatayo: Kudhibiti udanganyifu katika udahili uliotokana
na baadhi ya waombaji kutumia vyeti vya bandia, kuwapunguzia waombaji gharama
za kuomba udahili katika vyuo mbalimbali, kuondoa uwezekano wa mwombaji udahili
mmoja kudahiliwa zaidi ya mara moja na kuwanyima waombaji wengine nafasi,
kuiwezesha serikali kuwa na takwimu sahihi za waombaji udahili kwa ajili ya
kufanikisha mipango ya elimu nchini, na kuwawezesha waombaji udahili kujiunga
na mafunzo kwenye taasisi zinazotambuliwa na Serikali,” alieleza.
Dk
Rutayuga alieleza kuwa, kwa kutambua mafanikio ya udahili wa pamoja
yaliyopatikana, Serikali ya kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, imeamua kuwa maombi yote ya udahili kwa
ajili
ya mafunzo ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma) na Shahada ya
kwanza
(Bachelor Degree) yafanywe kupitia kwenye Mfumo wa Pamoja wa Udahili
(CAS).
Amefafanua kwamba. Baraza linautangazia umma kuwa, kuanzia mwaka wa masomo
2016/2017 udahili wa kozi zote nchini utafanywa kupitia Mfumo wa Udahili wa
Pamoja (CAS) unaosimamiwa na NACTE, Vyuo Vikuu
na taasisi za Elimu zote nchini Tanzania zinazotoa mafunzo ya Cheti na
Diploma kutodahili wanafunzi nje ya mfumo wa udahili wa Pamoja kuanzia mwaka wa
masomo 2016/17.
“Tunapenda kutoa taarifa pia kuwa, maombi ya kujiunga na kozi za Cheti na
Diploma yataanza kupokelewa rasmi kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja kuanzia
tarehe 4 Machi 2016, saa sita mchana. Baraza pia litaanza kupokea rasmi maombi
ya kujiunga na kozi za Shahada (Degree) kwa wahitimu wenye Diploma kupitia
Mfumo wa Udahili wa Pamoja kuanzia tarehe 4 Machi 2016, saa sita mchana,”
Kwa maelezo
zaidi ya jinsi ya kuomba mafunzo kwa kutumia Mfumo wa
Pamoja wa Udahili (CAS), alisema Baraza linashauri waombaji watembelee tovuti ya
Baraza ambayo ni www.nacte.go.tz.